Tuesday, March 20, 2012

Mtanzania aliyewahi kuwa Freemason ajitangaza,,,,,,,,,,Mtanzania Samwel ambae alitangaza kwenye NJIA PANDA ya CLOUDS FM kwamba amejiondoa FREEMASON sehemu ambayo anadai watu wanamuabudu shetani ameaplfy kwamba amewahi kuwashuhudia wasanii wakubwa wanne wa Tanzania ambao ni waumini wa dini hiyo.
Samwel amesema japo hawezi kuwataja hao wasanii majina, lakini aliweza kuwatambua kwamba ni Wawili wa bongofleva na wawili wa movie wote wa kiume, na ni wasanii wenye majina makubwa tu lakini kwa sasa wamekua hawajihusishi sana na usanii, wametingwa na vikao vya dini hiyo.
Ameamplfy kwamba alishawahi kukutana nao kwenye hilo kanisa Dar es salaam mara moja tu na mmoja kati ya wasanii hao aliingia kwenye ukumbi wa FREEMASON akiwa na gari aina ya Prado ambapo asilimia kubwa ya waumini ni wafanyabiashara.
Samwel anaedai kukaa ndani ya FREEMASONS kwa miezi tisa Amesema alikimbia na kujiondoa kwenye dini hiyo kwenye dakika za mwisho ambapo alikua amebakiza hatua moja tu apitishwa na kuingia kwenye list ya waumini wanaopewa utajiri na dini hiyo ila mwenzake waliekua pamoja ndio anakaribia kupewa utajiri sasa hivi.

Huyu ndio jamaa anaedai kuikimbia Freemason, hiyo alama hapo kwenye sikio anadai aliwekewa makusudi ili kurahisisha mambo wakati akifanya biashara ya dawa za kulevya.


Hii ndio alama anayodai kuwekwa akiwa FREEMASON, ni kama muhuri
Amesema katika ibada moja aliyoshiriki na hao wasanii walipovua nguo zote walizipeleka mbele na baadae kuzichukua baada ya ibada, kikubwa wanachokabidhiwa ni irizi ambayo inafanya kazi kutokana na amri ya aliekabidhiwa.
Samwel amesema uchawi kutoka kwenye dini hiyo upo kwa wafanyabiashara wakubwa ambapo hata kwenye baadhi ya mabasi yanayosafirisha abiria kumekua na michoro au alama za kishetani, huku mabasi mengine yakiwa yanachukua ule mchanga wa viatu ulioingia na abiria na kuufanyia mambo ya kishirikina baada ya abiria wote kushuka.
Anadai kwamba anafahamu vizuri kwamba amekua akitafutwa lakini anajificha na kukataa kupokea simu nyingi ambazo amekua akipigiwa, kwa sababu alijihusisha na biashara ya dawa za kulevya pia, biashara ambazo anadai hata wasanii hao wa bongo wanahusika kuzifanya huku wengine wakimiliki majumba ya kifahari AFRIKA KUSINI.

habari hii ni kwa hisani ya Millard Ayo's Blog

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...