Friday, April 27, 2012

Licha ya sajuki kuumwa ameamua kuingia mzigoni ili kuondokana na ugumu wa maisha,,habari hizi ni kwa hisani ya global publishers...

Licha ya kwamba afya ya msanii wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ bado hairidhishi kutokana na maradhi yanayomsumbua, juzikati staa huyo na mkewe Wastara Juma walinaswa ‘lokesheni’ wakiendelea kurekodi filamu yao.
 wanandoa hao Walinaswa wakiwa na baadhi ya wasanii maeneo ya Tegeta jijini Dar ambako walikuwa wakishuti filamu iliyopewa jina la Wakili huku Sajuki akiwa ndiye muongozaji.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Sajuki alikiri kuwa afya yake bado siyo nzuri lakini ameona badala ya kukaa ndani ni vyema akajishughulisha ili kukabiliana na ugumu wa maisha.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...