Wednesday, September 26, 2012

Cheka kidogo mdauu

Mdada mmoja mke wa mtu alikuwa akisumbuliwa sana na jamaa mmoja aliyekuwa akimtaka kila siku, hatimae akamwambia mumewe. Mume akamwambia mkewe, we kubali tuu, ila mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu.
Mdada akafuata masharti ya mumewe na hatimae wakaingia chumbani na yule bwana , mumewe akiwa tayari na panga uvunguni mwa kitanda. Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona ana makovu makubwa kifuani na mgongoni;
MKE: Heee mbona una makovu hivyo??
JAMAA: Niwe mkweli tuu, kwako dia!! mie nina tatizo sana la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania, nilishafumaniwa mara kumi na tisa, na wote walionifumania niliwaua. Ila jaribio la mwisho nilidakwa na mapolisi nikatumikia kifungo cha miaka 27 jela, Lakini ninavyopenda wake za watu sitaacha kuua. Hivi sina muda tangu nitoke huko jela hivyo nina ukame wa punda na nilipokuona moyo wangu ukakudondokea. Na nitatulia na wewe.
MKE: Heee! Haiwezekani jamani!!….jamaa akaendelea kuvua nguo alipomaliza mdada akaanza kujitahidi kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni aje kumuokoa, mume akabana kimya, kila mdada akijitihadi kupunga mkono hakupata jibu, mdada akalalamika kwa maumivu makali mpaka jamaa akamaliza shughuli zake akatokomea.
MKE: Huku akilia, ndio nini umenifanyia? Mbona hukutoka??
MUME: We we we, Weeeee mama naniii!!.. mwenyewe umesikia keshaua 19 ulitaka niwe wa ishirini?
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...