Tuesday, November 27, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA!!!



Msanii wa Bongo movie na mwanamziki Sharo milionea amefariki dunia leo hii kwa ajali ya gari alipokua akielekea Muheza, Tanga., kwa habari zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa movie Steve Nyerere, akiongea akiwa katika msiba wa msanii mwingine wa Bongo movie alifariki (John) kwa njia ya simu, akisikika kwa sauti ya masikitiko sana alisema
"ni kweli fetty sharo hatupo nae tena na nimeongea na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga na kuthibitisha habari hizo"akiongea na Clouds Fm, kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Bwana Constatine Massawe amesema " kifo cha Millionea kimetokea majira ya saa mbili, eneo linaloitwa Maguzoni songa , akiwa anaendesha gari aina ya toyota Harrier akitokea Dar  kuelekea Muheza, alipofika hapo gari liliacha barabara na kupinduka,na maiti imehifadhiwa katika chumba cha maiti ya  hospitali teule ya Muheza. alikuwa mwenyewe. Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi Amen
hii ni moja kati ya kazi alizowahi kuzifanya katika uhai wake 

2 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...