Wednesday, November 28, 2012

AMSHITAKI MKEWE KWA KUWA NA SURA MBAYA,ASHINDA KESI ALIPWA MAMILIONI


Mke wa Jian alivyokuwa awali kushoto na baada ya kufanya operesheni ya kurekebisha sura yake, kulia

Mwanaume mmoja nchini China alishtuka baada ya mkewe kuzaa mtoto mwenye sura mbaya na aliamua kumfikisha mkewe mahakamani kwa kutomjulisha kuwa sura yake nzuri ilitokana na operesheni za kubadilisha sura, alishinda kesi na kuzawadia fidia ya mamilioni.

Wakati Jian Feng alipomuona mtoto wake mchanga kwa mara ya kwanza alishtuka sana.
Mtoto wake huyo wa kike alikuwa na sura mbaya kiasi cha kwamba alishindwa kuamini kuwa mkewe aliyekuwa akionekana mrembo sana angeweza kuzaa mtoto kama huyo.

Jian alimgeuzia kibao mkewe na kumshtumu kuwa aliisaliti ndoa yao na kufanya mapenzi nje ya ndoa yaliyopelekea kuzaliwa kwa mtoto huyo.


Baada ya hali kuwa tata, mkewe alilazimika kutoboa siri kuwa urembo wa sura yake unatokana na operesheni zilizomgharimu zaidi ya dola 100,000 ili kuirekebisha sura yake aonekane mrembo. Mkewe alisisitiza kuwa mtoto huyo ni wa kwao.


Jian alikasirika sana kusikia hivyo na kuamua kumfikisha mkewe mahakamani akidai kuwa alirubuniwa kuingia kwenye ndoa na alidai fidia ya mamilioni ya pesa.


"Nilimuoa mke wangu kwa mapenzi makubwa kwa jinsi alivyokuwa akionekana lakini punde baada ya kufanikiwa kupata mtoto wa kwanza matatizo yalianza kwenye ndoa yetu", alisema Jian.


"Binti yetu alikuwa na sura mbaya sana kiasi cha kwamba nilitishika sana", Jian aliwaambia wanasheria wake kuwa mkewe alimvuta kwenye ndoa kwa kufanya operesheni ya kutengeneza sura yake aonekane mrembo na kuzaliwa kwa mtoto wao huyo ndiko kulikopelekea ukweli kujulikana.


Mahakama ilikubaliana na madai ya Jian na kuamua alipwe fidia ya dola 120,000 ( zaidi ya Tsh. milioni 170) baada ya mkewe kukiri kuwa hakuwahi kumwambia mumewe kuwa urembo wa sura yake unatokana na operesheni.


Mahakama ilimuona mkewe ana hatia ya kumrubuni Jian kuingia kwenye ndoa na ilikubali maombi ya Jian ya kuivunja ndoa hiyo.



2 comments:

  1. Write more, thats all I have to say. Literally, it seems as though you relied on
    the video to make your point. You obviously know what youre talking about, why throw away your
    intelligence on just posting videos to your weblog when you could be giving us something enlightening to
    read?

    Visit my page cellulite treatment cream

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...