Sasa wanawake wana uwezo wa kuamua kupata hedhi au la, baada ugunduzi wa vidonge ambavyo humfanya mwanamke asizione siku zake kabisa. Vidonge hivyo ambavyo vimefanyiwa majaribio kwa muda mrefu vimebainika kuwa na uwezo katika suala hilo. Kati ya wanawake waliotumia vidonge hivyo, asilimia 60 hawakuona kabisa damu kwenye siku zao, wakati asilimia 20 waliona vidoa tu. Hii ina maana kwamba, kati ya kila wanawake kumi wanaotumia vidonge hivi, wanawake wanane wanafanikiwa kutoziona siku zao.Vidonge hivyo vinavyofahamika kwa jina la Lybrel, ni vya kwanza duniani, ambavyo vimemudu kuondoa kabisa damu ya hedhi kwa mwanamke. Kampuni ya Wyeth Pharmaceuticals, ambayo ndiyo iliyofadhili utafiti huo, inasema vidonge hivyo ambavyo vitauzwa kwa bei rahisi na ambavyo hutumiwa kwa dozi ndogo havina madhara kwa watumiaji. Lakini hata hivyo naomba ieleweke kwamba kauli hiyo ni ya kutarajiwa sana kutoka kwa mtengenezaji wa bidhaa yoyote, iliyo au isiyo na madhara.
Lakini, wataaalamu wa masuala ya wanawake, wanasema mwanamke kuziona siku zake siyo lazima, yaani anaweza kuacha kuziona na hilo lisimletee madhara yoyote, labda tu kama ameacha kwa kuuugua. Mpaka sasa haijafahamika kama vidonge hivi vimeshaingia nchini, lakini naamini taarifa hii itapokelewa kwa furaha na si kwa wanawake tu, bali pia na wanaume ambao swala la hedhi kwa wake au wapenzi wao limekuwa kero.
Mnaweza Kubofya hapa kwa habari zaidi: http://contraception.about.com/od/prescriptionoptions/a/Lybrel.htm

Nawapenda sanaaa...
No comments:
Post a Comment