Friday, October 12, 2012

Jamani hii ni stori ya kweli inasikitisha sana ......soma utajifunza kitu...

Ilikuwa ni ajali kubwa na hata mimi sijui niliweza vipi kupona. Dereva na mke wangu walifia pale pale kwenye eneo la tukio. Tulikuwa tukitokea Chalinze kurudi Dar es salaam baaada ya kukagua shamba ambalo ilikuwa tulinunue katika kijiji cha Msata wilayani Bagamoyo. Mbele kidogo ya mji wa Chalinze ndipo ajali hiyo ilipotokea . Dereva wetu alikuwa akijaribu kulipita lori fulani lakini wakati huo huo gurudumu la mbele la gari letu lilipasuka na kusababisha gari kuyumba ambapo lililivaa lile lori. Kufuatia kuligonga huko, gari letu lilirudishwa katikati ya barabara ambapo liligongana uso kwa uso na gari lingine lililokuwa linakuja mbele yetu. Sikujua kilichotokea hadi baada ya siku mbili Muhimbili.

Nilipopata fahamu ilinichukua muda kukumbuka kidogo kilichotokea. Nilipouliza kuhusu mke wangu hakuna aliyesema kitu kati ya wale ndugu na jamaa zangu waliokuwa pale kando ya kitanda changu. Pamoja na maumivu yangu nilijua kilichokuwa kimetokea. Nilianza kulia, hata kabla hawajaniambia chochote. Kaka yangu aliponiambia "jikaze ni kazi ya Mungu, shemeji mama Rehema ametutoka." Nilipoteza fahamu. Nilipopata fahanu na kukubali kuipokea taarifa ile, niliambiwa kuwa mke wangu alifia pale kwenye eneo la ajali pamoja na dereva. Mimi nilikuwa nimevunjika mguu wa kushoto, mkono wa kushoto na mbavu mbili na kubanwa kifuani. Hali yangu kwa kweli haikuwa nzuri lakini nililazimika kujikaza. Mke wangu alikuwa amekufa, haikuwa rahisi kukubali.

Nilikuwa nampenda na yeye pia alikuwa ananipenda. Ukweli ni kwamba tulikuwa tukiaminiana sana na mke wangu ambaye nitamwita Sia {Jina linalokaribiana na jina lake halisi }. Tulikuwa tumeshibana kiasi kwamba, kulikuwa hakuna ambaye alikuwa hajui. Nilikumbuka kwamba kwa miaka minane ya ndoa yetu tulikuwa hatujawahi kukorofishana, ukiacha kusigishana kwa hapa na pale. Nilikuwa sijawahi kumsaliti na hata yeye pia. Nilijaribu kukumbuka ahadi zetu kwa kila mmoja na kuhusu watoto wetu wawili mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Kwa kweli ilinichukuwa muda wa saa kadhaa kukubali kwamba nilikuwa sina mke, mwili wa yule nimpendaye ulikuwa ukiganda mochuari. Nilijikuta nikiinuka kwa nguvu na kupiga yowe nikitaka kwenda kumfufua mke wangu. Nilikuwa nimechanganyikiwa kwa kweli! Ndugu zangu na jamaa waliokuwepo pale wodini walinishika na kunituliza.

Ilibidi waombe msaada kwa madaktari ambapo nilichomwa sindano iliyonipa utulivu na usingizi. Nilipoamka jioni sana , nilikuwa na utulivu kidogo, kaka yangu aliniomba nijikaze na kumrudia mungu, Aliniambia nijaribu kuukubali ukweli na hali halisi. Nilijikaza na aliniambia kwamba mazishi ya mke wangu ingebidi yafanyike kesho, kwa mujibu wa makubaliano ya ndugu wa pande zote. Aliniambia dereva wangu alikuwa amezikwa tayari na ndugu zake. Nilimwomba kaka wauache mwili wa mke wangu ili niwe nae karibu kwa muda fulani. Kaka alinishawishi sana nikubali kwa sababu, kama mwislamu ninajua inavyokatazwa kuuweka mwili wa marehemu bila kuuzika kwa muda mrefu, bila sababu.

Hatimaye nilikubaliana naye, lakini nilisema ni lazima nami niende kuzika. Kaka alinimbia kwa hali yangu nisingeruhusiwa na madaktari na wala nisingeweza kumudu kwenda makaburini Kinondoni. Nilimwambia kaka katika yote ningemkubalia lakini sio hilo la kutomzika mke wangu. Nilimwambia, habari ya madaktari aachane nayo na kuhusu mimi kumudu ningemudu tu. Nilikataa katakata hata kusikiliza ilibidi kaka aondoke pale bila muafaka. Walikuja ndugu zangu wengine kunishawishi lakini niligoma kabisa, hadi ikabidi wakubaliane nami.

Lakini walijua ingekuwa ngumu sana kutokana na hali yangu. Kesho yake walikuwa tayari wamepata ufumbuzi. Walikubaliana na uongozi wa hospitali kwamba nipelekwe makaburini kwa gari la wagonjwa. Ni kweli nilikwenda kuzika. Pamoja na kuwa waislamu huwa hatutoi heshima za mwisho kwa kuuona mwili wa marehemu, mimi nililazimisha hadi nikaonyeshwa mwili wa mke wangu. Alikuwa hana alama hata moja usoni kwani alikuwa ameumia miguuni hadi kifuani. Nilipomwona nilipoteza fahamu………… Tulimzika mke wangu na nikarudishwa hospitalini.

Nilitoka hospitalini baada ya mwezi mmoja na kurejea nyumbani. Nyumba yangu mwenyewe ilinitisha na nilihisi simanzi kubwa kuwa mle ndani. Watoto wangu walinisikitisha zaidi. Lakini nilishaamua kuikubali hali halisi. Nilikuwa nimekubali kuanza upya maisha. Siku ya Tatu tangu kurejea nyumbani niliamua kupangua ili kuvipanga upya vitu vya marehemu. Nilipanga nguo zake na mapambo mengine ya kike. Halafu ilibidi kupanga vitu vilivyokuwa kwenye droo zake ambazo funguo zake alikuwa nazo mwenyewe marehemu. Kwa sababu sikuwa najua alipokuwa ameweka funguo za droo zile mbili ilibidi nizivunje moja baada ya nyingine.

Droo ya kwanza ilikuwa na barua na karatasi mbali mbali za mawasiliano na mambo mengine. Hapo nilianza kuzisoma barua. Barua ya kwanza ilikuwa ni kutoka kwa mpenzi wake. Haikuwa ni barua ya zamani, kwani ilikuwa imetumwa kwake miezi minne tu kabla ya kifo chake. Ilitumwa na bwana aliyekuwa ametuuzia ile gari iliyohusika kwenye ajali iliyomuua. Sehemu ya barua ile ilikuwa imeandikwa:

Kuhusu hilo ni sawa mpenzi wangu.
Wewe mwambie nitawauzia kwa mkopo, tena kwa bei rahisi sana . Lakini hizo fedha utazichukua wewe. Kuhusu kwenda Harare nitakufahamisha, jaribu kwa upande wako kumwambia kwamba utakuwa na semina huko, April. Najua kufika Aprili tutaelekea huko. Nataka tuwe mahali huru na salama ili niufaidi mwili wako na wewe uumiliki wangu.

Barua hiyo ilijaa upuuzi mwingi……

Nilipomaliza kuisoma nilihisi kama ninayeota au ambaye nitaugua kichaa. Ni kweli huyu jamaa ndiye aliyetuuzia lile gari iliyochukua maisha ya mke wangu kwa bei ya chini sana . Gari Nissan Pajero kwa shilingi milioni 7.5 nzuri tu, hata kama imetumika! Kumbe ulikuwa ni mpango wake na mke wangu wa kuipatia familia yangu gari. Nilienda kupekua barua na hati kadhaa. Niligundua hati ya nyumba kwa jina la mke wangu.

Nyumba hii ilikuwa Kijitonyama. Nilipata barua nyingine. Hii ilikuwa ni ya bwana wake wa zamani lakini ilikuwa imeandikwa mwaka mmoja tu nyuma, ilikuwa ikimlaumu mke wangu kwamba hakuwa mkweli Sehemu muhimu katika barua hiyo ilikuwa imeandikwa:

Ninajua wazi huyo Rehema ni mwanangu na hata rafiki yangu Mudy amesema tunafanana sana . kama umeamua kunidanganya , ni sawa, lakini kumbuka hiyo ni damu yangu.
Sitamchukua wala kumdai lakini kujua ukweli ni muhimu kwangu.

Nilipomaliza kusoma barua ile nilishikwa na kizunguzungu. Nilitulia hapo kitandani kwa muda. Halafu niliendelea kupekua kwenye karatasi hizo. Niliona barua kadhaa na kadi za mapenzi.

Kadi mbili zilikuwa zinatoka kwa bosi wake. Barua moja ilikuwa ikitoka Uingereza kwa mtu aliyeitwa P Hughes. Huyu ni wazi alikuwa ni mpenzi wa mke wangu kwa muda mfupi, alipokwenda Uingereza miaka miwili nyuma kwa kozi fupi ya miezi sita. Barua yake ilikuwa imejaa sifa nyingi, akimsifia mke wangu kwa kuwa na mwili mzuri na kuwa mtaalamu wa mapenzi na ilisifia shanga zake pia.

Nilihisi nikibana kifua na mapigo ya moyo wangu yalikuwa kama yamesimama. Bila shaka siku ile ndipo yalipoanzia maradhi yangu ya shinikizo la chini la damu, ambayo ninayo hadi sasa. Nilivunja ile droo ya pili ambayo ilikuwa na picha kadhaa. Zote zilikuwa ni picha za mapenzi. Nilitazama mbili za kwanza, nikatoka chumbani mle nikiyumba.

Naomba nisiseme sana kuhusu picha hizi, kwa sababu, hata kama mtu sio mke wako, ni mwanamke unayemfahamu tu, ukiona picha zake akiwa kwenye hali kama ile, utatahayari sana . Picha unazoziona kwenye mikanda ya ibilisi au kwenye mtandao wa inteneti ndizo zilizokuwa pale kwenye droo, zikiwa ni za mke wangu na wanaume watatu tofauti.

Yule aliyejifanya kutuuzia gari na nyingine za wanaume wawili ambao sikuweza kuwafahamu. Baadae mchana baada ya kupata nguvu nilimpigia simu kaka mkubwa wa marehemu na kumwomba apite nyumbani. Huyu ni mtu wa hekima sana na hadi sasa tunaelewana sana.Alipofika nyumbani nilimwomba radhi na kumwonyesha barua na picha zile. Alizitazama kidogo na kunirudishia, alikaa kwa muda na kusema,
"Huyu sio dada yangu niliyekuwa namfahamu mimi, hii ni aibu kubwa sana shemeji." Hakuweza kusema chochote baada ya hapo, Alipoondoka kwa huzuni kubwa nilichukua nguo zote za mke wangu, barua, picha na vitu vingine vyote ambavyo vingenipa kumbukumbu yake na kwenda kuvichoma moto.

Nilivichomea moto shambani kwangu, Kiwangwa Bagamoyo na kufukia majivu yake. Tangu siku ile hadi leo sijakanyaga kaburini kwake, watoto wake wanakwenda na huwa nawahimiza kufanya hivyo. Yule mkubwa anajua mengi hivi sasa baada ya kusimuliwa na baadhi ya ndugu. Nilimwambia kwamba maneno yale hayana ukweli.

Lakini najua anafahamu kuwa yana ukweli, kwani kuna siku aliniiuliza, mbona haoni picha za mama yake ukutani. Nilimwambia, zinanitia uchungu zaidi. Ilibidi niende Afrika Kusini kupima DNA, ili kujua kama yule mtoto mdogo ni wangu kweli.

Bahati nzuri ilionesha kwamba ni wangu kwa asilimia kubwa sana. Hii ilinipa moyo sana . Kilichonitokea kimenifanya nisiwe na hamu hata ya kuwa karibu na mwanamke, achilia mbali kuoa.

Mtu ambaye umemuamini kuliko binadamu mwingine, kumbe ndiye anayefanya uasi usio na kipimo gizani. Nasema hivi mnapaswa kuwaamini wapenzi au wake zenu. Kilichonitokea mimi ni bahati mbaya na ninaamini kama marehemu angeendelea kuishi ni lazima ningekuja kumnasa.

7 comments:

  1. In fact no matter if someone doesn't know then its up to other visitors that they will help, so here it takes place.

    Look at my blog post: healthy diet plan

    ReplyDelete
  2. Wow that was strange. I just wrote an very lоng comment
    but afteг I clісked submit my
    comment didn't appear. Grrrr... well I'm not writіng all thаt over agаin.
    Regaгdless, just wanteԁ to say eхcellеnt blog!


    Also viѕit mу ωeblog make money online

    ReplyDelete
  3. Definitely consider that that you said. Your favourite reason seemed to be on the net the easiest factor to
    be mindful of. I say to you, I definitely get annoyed whilst people consider worries that they plainly do not recognise about.
    You managed to hit the nail upon the highest as neatly as outlined out the whole thing with no
    need side-effects , people could take a signal. Will probably be again to get more.
    Thank you

    Feel free to surf to my site Pure Garcinia Cambogia Reviews

    ReplyDelete
  4. No matter if some one searches for his necessary thing, so he/she
    wishes to be available that in detail, so that thing is
    maintained over here.

    Feel free to surf to my page: Apple stem cell serum review

    ReplyDelete
  5. Very nice post. I just stumbled upon your weblog and wished to say
    that I've really enjoyed surfing around your blog posts.
    In any case I'll be subscribing to your rss feed and I
    hope you write again soon!

    Also visit my web blog good modeling ()

    ReplyDelete
  6. I don't even know how I ended up here, but I thought
    this post was good. I do not know who you are but certainly you are going to a famous blogger if you are not already ;)
    Cheers!

    Also visit my site ... free dui attorney

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...