Wednesday, February 29, 2012

UWF KUMWINUA MWANAMKE MJASILIAMALI SIKU YA WANAWAKE DUNIANIPichani kushoto ni Bi Maryam Shamo ambaye ni Mratibu Miradi wa UWF, akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM kuhusu mchakato wa kumtafuta mwanamke mjasiliamali ambaye amejaribu kufuata nyayo za Mwanamakuka, ila kutokana na changamoto mbalimbali zinazomkabili amekwama kufikia malengo yake kupitia mradi wa Mwanamakuka chini ya chama kisicho cha kiserikali UWF (United of women friends) wameamua kumuwezesha mwanamke mjasiliamali ili kufikia malengo yake,kilele cha ukabidhiwaji wa tuzo hiyo ya Mwanamakuka itafanyika siku ya Wanawake Duniani,Machi 8 ,katika ukumbi wa Serena hotel zamani Movenpick,kulia kwake ni bi Jane Magembe ambaye ni Mratibu Msaidizi wa UWF.

Waratibu wa UWF wakiwa kwenye kipindi cha Leo tena  kuhusiana na tuzo ya Mwanamakuka,itakayotolewa kwenye hafla ya Siku ya Wanawake Duniani,itakayofanyika Machi 8 ndani ya Serena Hotel jijini Dar,kulia ni mwongozaji wa kipindi hicho Dina Marious


 2 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...